Kuhamasisha
Kupita Mashuleni na kutoa Elimu juu ya Arusha Teachers Saccos LTD. Kwa Lengo la Kuhamasisha Walimu ili waweze kujiunga
na chama, kwani ukijiunga na SACCOSS unakua mmiliki,Mteja na Muwekezaji Tofauti na Taasisi Nyingine.
Elimu ya Akiba.
Tutatoa Elimu Juu y Faida ya Kuweka Akiba Mara kwa Mara, Kuweka Hisa ya Lazima na Hiyari ili uweze kupata faida.
Elimu Ya Kukopa
Chama Kitaelimisha Walimu kuhusu tofauti ya kukopa SACCOSS na Taasisi nyingine zinazotoa mikopo. mfn: Ukikopa SACCOSS utaoata Gawio tofauti na taasisi Nyingine.
Riba Nafuu
Kupanga Viwango Vyenye Riba nafuu ili Wanachama waweze kukopa mikopo mbalimbali itakayowanufaisha.
Kutafuta Wataalamu
Kutafuta Wataalamu waliobobea kwenye Masuala ya Uwekezaji na ujasiriamali na ushirika kwa ujumla.
Huduma Bora
Kuhakikisha Kila Mwanachama Anapata Huduma Bora Zitakazomfaidisha ili kila Mwanachama awe na Maisha Bora