Malengo Makuu ya Arusha Teachers SACCOS Ltd

Icon
i

Kuhamasisha Walimu wote wa Arusha wawe wamejiunga na chama ifikapo 2025

Icon
ii

Kuhamasisha uwekaji wa Akiba, Hisa na Amana ili kuendeleza na kukuza mtaji wa Chama.

Icon
iii

Kutoa Elimu kwa jamii nzima ili kujua umuhimu wa kujiunga na SACCOSS

Icon
iv

Kujengea uwezo wanachama ili kutoa Mikopo yenye riba nafuu ili kuwainua Kiuchumi.

Kuhusu Sisi

Arusha Teachers SACCOSS LTD.

Hiki ni Chama cha Kuweka na Kukopa cha Walimu wa Halmashauri ya Jiji la Arusha. Kilianzishwa tarehe 23 mwezi Julai mwaka 1997 na kupewa namba ya kuandikishwa AR.329. Kikiwa na wanachama 50, ambapo wanawake ni 38 na wanaume ni 12. Lengo kuu likiwa ni kumkomboa mwalimu wa shule za awali, shule za msingi, shule za sekondari na vyuo kuweza kujiwekea akiba na kupata mikopo yenye riba nafuu ili kujiinua kiuchumi na kijamii. Chama kimepata leseni kutoka Tume ya Maendeleo ya Ushirika yenye namba PRI-ARS-ARS-CC-2022-854. Arusha Teachers SACCOS kina leseni ya daraja A.

Piga Simu

Misingi ya Chama

Ushirikiani/Mshikamano

Mfanikio ya Chama yatakuwepo endapo kutakuwepo na ushirikiano na Mshikamano wa karibu kati ya Wanachama, Bodi ya watendaji na wadau wake. ni wajibu wa kila mdau kutoa ushirikiano pale unapohitajika.

Uwajibikaji

Viongozi wa Chama, Wanachama na watendaji wanapaswa kuwajibika kwa maslahi mapana ya Chama.

Kujali Wanachama

Mara zote Viongozi wa Chama na watendaji wake watapaswa kutoa Huduma iliyo bora kwa wanachama wake.

Uwazi

Shughuli za Chama Zitaendeshwa katika Hali ya Uwazi na kuzingatia misingi ya kumlinda mwanachama pamoja na kuzingatia Sheria,Kanuni na muongozo wa chama.

Ustadi

Bodi pamoja na watendaji watapaswa kuzingatia na kufuata viwango vya kitaalamu walivyonavyo wakati wa kuendesha shughuli za chama.

Uaminifu

Viongozi wa chama pamoja na watendaji wanapaswa kua waaminifu wakati wa kuendesha shughuli za Chama.

Maono

Maono Ya Chama

MUUNDO WA CHAMA

i. MKUTANO MKUU

Hiki ndicho chombo kikuu cha maamuzi katika chama.

ii. BODI YA CHAMA

Ndicho chombo kinachosimamia shughuli zote za chama na inachaguliwa na mkutano mkuu kwa mujibu wa masharti ya chama.

iii. MANEJIMENTI YA CHAMA

Ndicho chombo chenye wajibu wa utendaji wa shughuli zote za chama kikiongozwa na Meneja wa chama kwa mujibu wa masharti ya chama.

iv. KAMATI YA MIKOPO

Ni kamati itakayokuwa na wajumbe watatu kutoka kwenye bodi ambao watakuwa na jukumu la utoaji mikopo na ufuatiliaji wa mikopo na kutoa taarifa ya mikopo kwa bodi kwa mujibu wa masharti ya chama.

v. KAMATI YA USIMAMIZI

Ni jicho la wanachama katika shughuli zote za chama na inachaguliwa na wanachama kwenye mkutano mkuu kwa mujibu wa masharti ya chama.

HUDUMA YA KUHIFADHI FEDHA

Tunajali usalama na ustawi wako wa kifedha

HISA

  • i. Kila mwanachama anatakiwa kuwa na hisa 50 zenye thamani ya Sh.500,000. HISA 1 INA THAMANI YA SH. 10,000/-.
  • ii. HISA NDIO INAMFANYA MWANACHAMA AWE MMILIKI WA CHAMA.
  • iii. Kila mwanachama atapata gawio la faida ya hisa kwa mwaka kiasi cha 40% ya faida ya chama baada ya kutoa mafungu ya akiba ya lazima.




AKIBA

  • i. Kila mwanachama anawajibika wa kuchangia akiba kila mwezi kiasi kisichopungua Sh.50,000/-.
  • ii. Akiba itamwezesha mwanachama kukopa mkopo mara 3 ya akiba alizojiwekea.
  • iii. Mwanachama atapata faida juu ya akiba kila robo mwaka kwa faida itakayopatikana kwa kiasi cha 4%.
  • iv. Mwanachama ataruhusiwa kupunguza ¼ ya akiba yake kwa mwaka mara moja na kama hana mkopo.
  • v. Kila mwanachama atapata gawio la faida ya akiba kwa mwaka kiasi cha 30% ya faida ya chama baada ya kutoa mafungu ya akiba ya lazima.

KUJIUNGA NA CHAMA CHA ARUSHA TEACHERS SACCOS LTD

Fuata hatua hizi ili kuwa mwanachama

MASHARTI YA KUJIUNGA

  1. i. Kujaza fomu ya maombi ya kuwa mwanachama.
  2. ii. Kuwa na picha mbili 'passport size'.
  3. iii. Kuwa na salary slip itakayoonyesha upatikanaji wa makato ya akiba.
  4. iv. Kuleta namba za NIDA, TIN number, tarehe ya kuzaliwa, namba za simu na TIN number pamoja na barua pepe.
  5. v. Kuandika warithi wake wawili.
  6. vi. Kulipa kiingilio cha Sh. 30,000/=.
  7. vii. Kulipa HISA 1 yenye thamani ya Sh. 10,000 na HISA zilizobaki 49 zenye thamani ya Sh. 490,000/- kumalizia kulipwa ndani ya miezi sita.
  8. viii. Kulipa akiba ya kuanzia Sh. 50,000/=.
  9. ix. Kulipa fedha ya jengo Sh. 65,000/=.
  10. x. Kununua sare ya chama Sh. 16,500/-.
  11. xi. Na kununua masharti ya chama kwa Sh. 5,000/-.

Lazima uwe mwalimu wa Halmashauri ya Jiji la Arusha na uwe na cheki namba ili chama kiweze kupata makato yako na uwe mwaminifu, mtiifu mwenye ushirikiano na wenzake.

MKOPO

Maelezo kuhusu huduma za mikopo

  1. Kuna aina mbalimbali ya mikopo, kama vile mkopo wa biashara, elimu, ujenzi, na kilimo. Mikopo yote hiyo inatolewa kwa riba ya 14% 'reducing balance'. Muda wa kulipa ni kuanzia mwezi mmoja hadi miezi 60 jinsi mwanachama atakavyoamua.
  2. Mkopo wa dharura ni 500,000/-, na riba yake ni 10%. Mkopo huu unarudishwa ndani ya miezi 6. Kila mwezi utakaosababisha ucheleweshaji wa mkopo wa dharura utatozwa adhabu ya Sh. 30,000/-.
  3. Mwanachama atakopa mara 3 ya akiba yake kwa kuzingatia makato katika salary slip yake.
  4. Mwanachama anaweza kufanya 'top up' ya mkopo wake na kuomba mkopo mpya.
  5. Dhamana ya mkopo ni mshahara kwa walimu wa serikali na wale walimu waliochama wa shule binafsi na wastaafu wataweka dhamana mali isiyohamishika.
  6. Ada ya fomu ni 0.1% ya mkopo unaochukua na mkopo wa kuanzia Sh. 1,000/- hadi Sh. 1,000,000/-. Ada ya fomu ni Sh. 1,000/-.
  7. Kila mwanachama atapata gawio la faida ya mkopo aliokopa wa mwaka husika kiasi cha 30% ya faida ya chama baada ya kutoa mafungu ya akiba ya lazima.
  8. Fomu za mikopo zinapitishwa mara 1 kwa mwezi tarehe 15.

MFUKO WA MAJANGA NA RAMBIRAMBI/MAJANGA

Maelezo kuhusu mfuko wa majanga na rambirambi/majanga

MFUKO WA MAJANGA

Ni mchango unaolipwa mara moja unapokopa mkopo kiasi cha 1.5% ya mkopo anaokopa mwanachama, ili kuwa kinga ya majanga ya kifo. Ikitokea mwanachama aliyekopa atafariki dunia, mfuko huu wa majanga utalipa deni lililobaki.


RAMBIRAMBI/MAJANGA

  1. Pindi mwanachama akifariki, chama kitatoa rambirambi ya Sh. 500,000/- kwa familia ya marehemu.
  2. Mwanachama akipata janga la moto au mafuriko na wajumbe wa bodi kujiridhisha, atapewa Sh. 500,000/- kama pole ya majanga.

ADHABU

Adhabu mbalimbali katika Chama cha Arusha Teachers SACCOS Ltd.

  1. MWANACHAMA AKIPOTEZA KITABU ITAMLAZIMU KULIPA KIASI CHA SH.20,000/- ILI AWEZE KUJAZIWA KITABU KINGINE.
  2. MWANACHAMA AKICHELEWESHA KULETA KITABU KIJAZWE ZAIDI YA MIEZI MIWILI (2) ATATOZWA ADHABU YA SH. 1,000/- KILA MWEZI ALIOCHELEWESHA.
  3. MWANACHAMA ASIPOHUDHURIA MKUTANO MKUU BILA TAARIFA ATATOZWA KIASI CHA NAULI YA SIKU HIYO INAYOLIPWA KWA WANACHAMA.
  4. KUNA ADHABU ZITATOZWA KULINGANA NA MAAZIMIO YA MKUTANO MKUU MF. UKIWA UNADAIWA MKOPO, HISA AU AKIBA NA HUJALIPA KWA WAKATI UTAKATWA NAULI YAKO NA KUBAKIZIWA KIASI CHA SH. 10,000/- TU.

MOTISHA & MIFUMO

Motisha na mifumo inayotumika katika Chama cha Arusha Teachers SACCOS Ltd.

MOTISHA

KILA MWANACHAMA AKIFANIKIWA KUMWINGIZA MWANACHAMA MPYA ATAPEWA MOTISHA YA SH. 10,000/-

MIFUMO

CHAMA KINATUMIA MFUMO WA FORESIGHT NA MUVU (MFUMO WA MAENDELEO YA USHIRIKA TANZANIA NZIMA).

WASIMAMIZI NA WADAU

Wasimamizi na wadau muhimu katika Chama cha Arusha Teachers SACCOS Ltd.

WASIMAMIZI

  1. MAAFISA USHIRIKA HALMASHAURI YA ARUSHA
  2. AFISA USHIRIKA MKOA
  3. MRAJIS MSAIDIZI MKOA
  4. MRAJIS MKUU TAIFA

WADAU

  1. CHUO KIKUU CHA USHIRIKA MOSHI
  2. SCCULT
  3. TFC
  4. NA WADAU WENGINE KWA MUJIBU WA SHERIA YA VYAMA VYA USHIRIKA

Wasiliana Nasi

Je Unahitaji Msaada? Karibu!

Kwa Mawasiliano Zaidi kwa ajili ya taarifa kuhusu chama chetu na pia kama unahitaji kujiunga na chama chetu karibu sana na usisite kutupigia simu.

+255 759 800 221

Uongozi

Viongozi Wetu

Mwendaeli Kisaka
Mwenyekiti
Edna Laiser
Meneja